Watu Quotes

Quotes tagged as "watu" (showing 1-30 of 81)
Enock Maregesi
“Be nice to the environment. Be nice to animals. Be nice to people. If you do that, you will leave a mark on the world.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitaka watu wakuheshimu usitumie mabavu. Tumia hekima. Maana, watu hawaheshimu wewe ni nani au unatoka wapi, wanaheshimu nguvu ya matendo yako. Kama una tatizo na mtu usichukue uamuzi wa haraka. Ongea na watu kupata hekima.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiongozi kwa sababu ya haki akibarikiwa na Mungu, hata watu anaowaongoza watabarikiwa na Mungu pia. Lakini kama kiongozi amelaaniwa na Mungu kwa sababu ya uovu, hata watu anaowaongoza watalaaniwa pia.”
Enock Maregesi

“Ukionyesha maisha ambayo si yako kwa watu, ujue unajipotezea muda wako pasipo kujijua. Waache watu waone wenyewe.”
Simon Mashalla

Enock Maregesi
“Isipite siku hata moja katika maisha yako bila kusema hata kimoyomoyo kwa wazazi wako na kwa watu wote wanaokupenda kwamba unawapenda, kwani siku moja hawatakuwepo tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kumbuka kwamba watu wanaokupa pesa bila masharti yoyote wanajisikia vizuri sana kufanya hivyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hutaweza kumiliki watu bila damu ya Mwanakondoo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiongozi wa wananchi au wa serikali hapaswi kuchaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, anapaswa kuchaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika nchi kama kiongozi wa dhima aliyokabidhiwa kwa unyenyekevu na heshima kwa wananchi wenzake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usipoangalia kwa undani sana, mapepo wanatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kuwaona. Aidha, wanaweza, bila hata sisi kujua, kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi. Watu wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani na mapepo wake hawataki tujue kama wanatudanganya au wameshatudanganya tayari, na hawataki tujue kama wako hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini. Licha ya hili jambo kutokea katika maisha yetu, Shetani bado anaweza kutudanganya hadi pale tutakapoerevuka kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kwamba udanganyifu huo hautatokea tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hata hivyo, Shetani anaweza kutudanganya kupitia tamaduni zetu tulizozaliwa nazo. Utamaduni, dunia tunapoishi, ndiyo chanzo cha udanganyifu huu. Yesu Kristo alikufa msalabani ili tupate uhuru kutoka kwa Shetani. Chukua hatua sasa kwa sababu Shetani anaweza kukuteka, na kukufanya mtumwa tena.”
Enock Maregesi

“Sijawahi ona silaha kali na nzuri kama ukweli. Ukiwa mkweli utaipenda tu. Watu wanaogopa ukweli kwa sababu ya makali yake ndiyo maana waongo.”
Simon Mashalla

Enock Maregesi
“Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani. Mafanikio hayapimwi kwa pesa au mali kiasi gani unayo, mafanikio yanapimwa kwa amani ya moyo au maisha ya watu kiasi gani umeboresha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unapofikia hatua ya kuwa na kila kitu katika maisha, unapokuwa umefanya kila kitu ulichotamani kufanya katika maisha, unakuwa na bahari nzima ndani ya tone ambalo ni wewe. Unaridhika. Wewe si tone tena ndani ya bahari, wewe ni bahari ndani ya tone. Kinachobaki baada ya hapo ni kusaidia jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo, kuacha alama katika dunia kabla na baada ya wewe kuondoka, bila kujali watu watasema nini juu ya maisha yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Boresha maisha ya watu kwa kadiri utakavyoweza. Ukisaidia mtu 1 watahurumiwa watu 10. Ukisaidia watu 10 watahurumiwa watu 100. Ukisaidia watu 100 watahurumiwa watu 1000. Kila mmoja wetu akitambua wajibu wake katika jamii, Mungu atatuhurumia sisi wote. Maisha ya mtu mmoja yakiboreka, mmoja huyo ataboresha na ya wengine wengi. Hivyo, endelea kuogelea lakini usisahau kurudi nyuma katika jamii.”
Enock Maregesi

“Oga. Watu hawaogi ndiyo maana wachafu. Kuoga ni lazima kutumia maji. Ukitaka kuoga neno, tumia maji; na ukitaka kuoga maji, tumia neno; kuwa msafi. Huwezi kuyakimbia maji maana usipooga utanawa, na usiponawa utayanywa tu. Maji ni neno na neno ni uhai wa maji.”
Simon Mashalla

“Nilipozaliwa nilipendwa na kuogopwa, watu walicheza na mimi lakini mimi sikucheza nao. Niliwapenda.”
Simon Mashalla

Enock Maregesi
“Watu wakiwa wamekasirika ongea nao jibu; usiongee nao tatizo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu haamui jinsi watu wanavyoamua. Mtu akikwambia huna kipaji muulize yeye ni nani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wengi hawana uelewa ndiyo maana hawajui.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usidharau midomo ya watu. Kuna watu wanaona mbele.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dunia hii ina watu ambao Mungu anataka kuwaokoa, lakini inafanya wawe wagumu kwelikweli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna tofauti kati ya haki na utawala wa mabavu. Haki ni jambo ambalo mtu anastahili au kitu anachostahiki kuwa nacho. Utawala wa mabavu ni utawala wa kidikteta. Ukitenda haki lazima kuna watu watafaidi. Lazima kuna watu wataumia. Fidel Castro alikuwa kiongozi msahili. Alikuwa kiongozi aliyewezesha kutendeka kwa mambo. Kwa sababu hiyo, wachache walimpenda, wengi walimchukia. Lakini ili ufanye mazuri lazima upambane na mabaya. Shetani mwenyewe hatakuruhusu ufanye mazuri bila kukuletea mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna watu hawaamini kama Mungu yupo, lakini maisha yao yanaamini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama umechagua mtu akashinda au akashindwa na matokeo yakatangazwa, idadi kubwa ya watu ikakubaliana na matokeo hayo, umeongea na nchi yako na imekujibu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika karne iliyopita, wanaakiolojia waligundua mbegu za pamba na ngano katika baadhi ya makaburi waliyokuwa wakiyafukua kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi. Mbegu hizo, zilizokadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 2000 hadi 4000, zilimea na kukua zilipopandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Roho ya maisha ilikuwa bado imo ndani ya mbegu hizo, pamoja na kwamba zilikosa mvua na jua kwa zaidi ya miaka 2000.

Huu ni uthibitisho kwamba kama mbegu itapandwa, itamea na kukua kama itapandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Matumizi sahihi, watu ni ardhi na mazingira yetu na kile tunachokifanya baada ya kupanda mbegu ni neno la ukweli ambalo ndani yake kuna kanuni na mafundisho ya Mungu, ndicho kinachoathiri matumizi ya mbegu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wote ni wa Mungu, watu ni matatizo. Wewe huna mtu, lakini bado unapambana na Mungu kuhusu watu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kinachosababisha tupambane na Mungu ni matatizo, ambayo huletwa na watu, na tunapambana kwa silaha ya uongo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unataka kufanikiwa lakini hutaki watu wakuone. Kama una kipaji kionyeshe kwa watu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dunia ni mbaya kwa sababu sisi wenyewe ni wabaya. Vitu ambavyo ni viovu ndivyo tunavyovipenda zaidi kuliko vinavyotustahili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ubinadamu una kila kitu isipokuwa upendo miongoni mwa watu.”
Enock Maregesi

« previous 1 3