Mtu Quotes

Quotes tagged as "mtu" (showing 1-30 of 54)
Enock Maregesi
“Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lolote unalolifikiria yupo mtu mahali fulani duniani ameshalifikiria.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usimdharau mtu aliyesaidia kukupa kazi ulipokuwa huna kazi, wala usimdharau mtu aliyesaidia kukulea ulipokuwa mdogo, au mtu aliyeokoa maisha yako au mtu aliyekusaidia kwa namna yoyote ile. Ukimdharau, utakaposhuka, atakusaidia kwa rehema za Mwenyezi Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tunapaswa kuyafikiria madhaifu yetu na dhambi zetu kwa makini sana, kwa kiasi cha kuyashinda madhaifu hayo na dhambi hizo, kabla hatujatoa maamuzi makali dhidi ya wenzetu. Tunawezaje kumlaumu mtu wakati hata sisi wenyewe tunaweza kuwa na matatizo makubwa? Tusiwe wanafiki. Badala ya kulaumu, saidia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mheshimu sana mtu aliyekupandisha juu kwa sababu utakaposhuka ndiye atakayekupokea, ijapokuwa unaweza usishuke kabisa au unaweza kushuka ukapokelewa na mtu mwingine baki, kwa kudura za Mwenyezi Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna vitu vitatu ndani ya mtu: kuna hiari, kuna ufahamu, na kuna mwili. Hiari inatawaliwa na Mungu; ufahamu unatawaliwa na malaika mwema; mwili unatawaliwa na nyota lakini chini ya usimamizi wa malaika wema: malaika wema walisimamisha jua na mwezi kwa ajili ya Yoshua na wana wa Israeli juu ya Gibeoni na katika bonde la Aiyaloni, walirudisha jua nyuma kwa ajili ya Hezekia mfalme wa Yuda na kwa ajili ya nabii Isaya, na waliifanya dunia ‘kuvaa koti’ ghafla wakati wa kusulubiwa kwa Mwanakondoo wa Mungu Anayeondoa Dhambi. Moyoni ni mahali patakatifu. Hata malaika wema hawawezi kuona ndani ya moyo wa mtu, ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya hivyo, na alichokihifadhi Mungu ndani ya moyo huo ni hiari ya mtu ya kuchagua mema au mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hana uwezo wa kupandikiza chuki au upendo au kitu chochote ndani ya moyo wa mtu, bila mtu mwenyewe kupenda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya moyo wa mtu, binadamu angeshatengeneza moyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tunazaliwa, kuteseka na kufa kwa sababu ya dhambi ya asili ya wazazi wetu wa kwanza (Adamu na Hawa). Kama Hawa asingekubali kudanganywa na Shetani, tungezaliwa bila uchungu, tungeishi bila kuteseka na tusingekufa milele. Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Mungu Ahusiki na dhambi, Ahusiki na mwili, Anahusika na roho. Hivyo, mtu anapofariki mwili unabaki duniani lakini roho inarudi kwa Mungu; kwani Yeye ndiye aliyeitengeneza na kuiweka katika moyo wa mtu. Mimi na wewe ni viumbe vyenye thamani kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu; mapenzi Yake kwetu hayana masharti yoyote. Hainiingii akilini (hata kidogo) kumtesa mtu unayempenda kiasi hicho milele, wakati uwezo wa kumwokoa unao.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ina thamani pale unapokuwa nayo, si pale unapokuwa huna, hivyo iweke mahali unapoweza kuiona: katika nyumba, katika shamba au katika elimu. Badala ya kumpa mtu pesa ili ajenge nyumba, mpe nyumba. Badala ya kumpa mtu pesa ili afanye biashara, mpe biashara. Halafu, mpe elimu afanye maamuzi ya biashara yake. Pesa ina laana na Mungu pekee ndiye anayeweza kuiondoa laana hiyo. Ni rahisi kwa tajiri kupata baraka ya pesa kwa sababu ana pesa na ana uwezo mkubwa wa kusaidia maskini. Ni vigumu kwa maskini kupata baraka ya pesa kwa sababu hana au ana uwezo mdogo wa kusaidia maskini. Mungu anaweza kuondoa laana ya pesa kupitia hisani kwa maskini, kitu ambacho aghalabu hufanywa na matajiri wenye uwezo mkubwa. Heri kutoa kitu au huduma au elimu kwa maskini kuliko pesa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu akikupa pesa kwa ajili ya kufanyia kitu kibaya chukua. Kisha ipeleke polisi, ambapo utatoa taarifa zake pia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usimdharau mtu aliyesaidia kukusukuma juu katika ngazi ya mafanikio yako, ikiwa utafanikiwa, kwa sababu kuna leo na kesho. Ukishuka, kama ulimdharau, hatakuamini tena. Lakini ukishuka, kama ulimheshimu, na kama bado ana uwezo wa kukupandisha juu, atakupandisha tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sipendi dharau: mimi kumdharau mtu au mtu kunidharau mimi. Sitakudharau kwa sababu sikujui. Hupaswi kunidharau kwa sababu hunijui.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Boresha maisha ya watu kwa kadiri utakavyoweza. Ukisaidia mtu 1 watahurumiwa watu 10. Ukisaidia watu 10 watahurumiwa watu 100. Ukisaidia watu 100 watahurumiwa watu 1000. Kila mmoja wetu akitambua wajibu wake katika jamii, Mungu atatuhurumia sisi wote. Maisha ya mtu mmoja yakiboreka, mmoja huyo ataboresha na ya wengine wengi. Hivyo, endelea kuogelea lakini usisahau kurudi nyuma katika jamii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Endeleza nafsi yako katika kujitegemea, kwani ukishaifundisha nafsi yako kujitegemea hutamtegemea mtu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Utamsaidiaje mtu aliyekukosea? Msamehe!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu haamui jinsi watu wanavyoamua. Mtu akikwambia huna kipaji muulize yeye ni nani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu akikuomba msamaha msamehe. Usipomsamehe hutasamehewa na aliyetusamehe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unapotenda wema kwa mtu au kitu huwezi kujua ni kitu gani kizuri au kibaya kitatokea kwako au kwa mtu mwingine baadaye kupitia wema ulioutenda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kipaji cha mtu huwezi kushindana nacho. Ukijaribu kushindana nacho unajaribu kushindana na kitu kilichoshindikana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Si rahisi kumkamata mtu anayeandamana moyoni mwake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Bila kujali dini ya mtu, bila kujali anaamini nini, kila mtu anatakiwa kujua kusudi la maisha yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiua mtu damu yake itakusuta maisha yako yote! Itaongea na wewe ikikulaumu milele!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu anayejaribu kupambana na Mungu anajaribu kupambana na jambo lisilowezekana. Hatakuwa na uwezo wa kushinda. Kufanya hivyo ni upumbavu usioweza kuelezeka, lakini wanadamu hatukomi kufanya hivyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wote ni wa Mungu, watu ni matatizo. Wewe huna mtu, lakini bado unapambana na Mungu kuhusu watu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna daktari anayeweza kuponya saikolojia ya mtu. Saikolojia ya mtu huponywa na mtu mwenyewe; nje ya ufahamu wa kawaida.”
Enock Maregesi

« previous 1