Uhuru Quotes

Quotes tagged as "uhuru" (showing 1-11 of 11)
Enock Maregesi
“Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wape watoto uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa shaghalabaghala.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tunasema uongo kwa sababu hatuna ujasiri wa kusema ukweli. Ukweli hautupi uhuru, unatupa upweke.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukisema ukweli utapata uhuru wa nafsi. Ukisema uongo utapata uhuru wa umma. Heri uhuru wa nafsi kuliko wa umma.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watoto hawatakiwi kuchungwa kupita kiasi hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho. Uhuru utakaowanyima wakiwa wadogo watakuja kuutafuta baadaye wakiwa wakubwa. Wakiutafuta baadaye wakiwa wakubwa hawataeleweka vizuri katika jamii. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata lakini si uhuru wa kila kitu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa bendera ya taifa letu! Alikuwa alama ya amani, haki, uhuru, ujamaa, uzalendo, na Tanzania.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shahidi mwaminifu na wa kweli anayajua mambo yetu yote tangu kuumbwa hadi mwisho wa dunia yetu. Kwa hiyo, ni kweli unabii lazima utimie. Mungu anataka tuwe na amani ndani ya mioyo yetu lakini anajua si jambo rahisi kwa sababu ya hila za Shetani. Shetani asingekuwepo amani ingekuwepo; watakatifu wasingekuwepo, dunia isingekuwepo. Lakini mlango wa rehema bado haujafungwa. Bado tuna uhuru wa kuchagua mema dhidi ya mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hata hivyo, Shetani anaweza kutudanganya kupitia tamaduni zetu tulizozaliwa nazo. Utamaduni, dunia tunapoishi, ndiyo chanzo cha udanganyifu huu. Yesu Kristo alikufa msalabani ili tupate uhuru kutoka kwa Shetani. Chukua hatua sasa kwa sababu Shetani anaweza kukuteka, na kukufanya mtumwa tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ni mtakatifu na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi wala hatesi. Tunajiua na kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua mema au mabaya. Lakini anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu pale tunapoenenda sawasawa na machukizo yake. Damu ina nguvu kuliko Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza kukudhuru. Lakini usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani atakuona. Hivyo, atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa ameruhusu akudhuru, kwa sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya aliotupatia, ijapokuwa ana uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo Mungu anakuwa ametoa adhabu kwa binadamu.”
Enock Maregesi