Yesu Kristo Quotes

Quotes tagged as "yesu-kristo" (showing 1-30 of 38)
Enock Maregesi
“Biblia pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo.

Mathayo alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo.

Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu.

Yohana alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu, kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa. Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani.

Petro alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake Yesu Kristo.

Yakobo ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki wa hekalu aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini) na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo.

Yakobo mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo hajamwita kuwa mchungaji wa Injili yake. Kama kiongozi wa kanisa hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi wa Yesu Kristo.

Bartholomayo, ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia. Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo.
Bartholomayo aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki.

Andrea alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia msalaba huo kwa maneno yafuatayo: "Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake." Aliendelea kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka akaishiwa na nguvu na kuaga dunia.

Tomaso alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika bara la India.

Mathiya alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa. Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa.

Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo.

Mitume walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo, na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia iliandikwa na mitume.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Jina la Yesu ni kubwa kuliko majina yote duniani na hata kuzimu. Lazima Shetani aliogope kuliko anavyomwogopa Bikira Maria au sakramenti za aina zote. Kumbuka, jina la Yesu halitajwi kilingeni. Linatajwa kanisani, ambapo linatajwa kinafiki. Hivyo, aliye na mamlaka ya kuaminiwa na kuabudiwa na aponyaye ni Yesu Kristo peke yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sabato ilianzishwa na Mungu siku ya saba ya uumbaji wake. Siku ya Sabato ni siku takatifu, iliyoko katika Amri Kumi za Mungu, ambayo hatuna budi kuitunza na kuiheshimu. Sheria ya Siku ya Sabato haikufa baada ya kifo cha Yesu Kristo msalabani kama Wakolosai wanavyodai. Wakolosai walifuata falsafa za kipagani, na walizileta falsafa hizo ndani ya mwili wa Kristo ambalo ni kanisa. ‘Usiiamini’ Wakolosai 2:17. Iamini Wakolosai 2:20-23, ambapo Paulo anafundisha Mataifa jinsi ya kuitunza Sabato, na 1 Wakorintho 12:27 ambayo inatoa maana halisi ya Wakolosai 2:17. ‘Mwili wako ni wa Kristo’ ni tofauti na ‘mwili wa Kristo’ na ni tofauti na kanisa. Ukiamini kama mwili wako ni wa Kristo na ni kanisa, utaitunza Sabato.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini damu na maji vina maana kubwa katika maisha yetu. Biblia inaeleza kuwa wakati Yesu Kristo akiwa msalabani alichomwa ubavu wake kwa mkuki, ikatoka damu na maji, ndipo zilipozaliwa sakramenti za kanisa. Aidha, tukio la askari wa Kirumi kumchoma Yesu na damu na maji kutoka lina maana nyingine kubwa katika maisha yetu. Hapo ndipo Ukristo ulipozaliwa; na ni kwa sababu hiyo mwanamke anapojifungua hutoa damu na maji kutokana na kupasuka kwa utando wa mfuko wa uzazi. Kutokana na hayo, Wakristo wanapoabudu msalaba wanaeleza umuhimu wa matukio na mafundisho waliyopata kupitia mateso aliyopata kiongozi wao na kuwa, msalaba ni chombo cha ukombozi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y. Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo, katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo. Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa. Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi hivi ndivyo wanavyoapishwa na kuikana imani ya Kikristo: Mwanafunzi hupelekwa kilingeni katika siku maalumu kuonana na Shetani, pamoja na jopo la wachawi. Shetani hutokea katika mwili wa hewa, mwili uliochanganyikana na hewa na mvuke mzito, wa mwanamume na kuwasihi waishikilie imani yao kwake kwa mioyo yao yote, huku akiwaahidi utajiri na maisha marefu kama hawatamkana. Kisha wachawi wanampendekeza mwanafunzi kwa Shetani. Shetani humuuliza mwanafunzi kama yuko tayari kuikana imani yake, kuachana na Ukristo na kutokumwabudu Mwanamke Aliyebarikiwa Kuliko Wanawake Wote Duniani Maria Magdalena, na kutoziheshimu sakaramenti za aina zote. Mwanafunzi atakapokubaliana na masharti hayo, Shetani atanyoosha mkono wake na kumsihi mwanafunzi anyooshe wa kwake. Kwa mkono wake mwenyewe, mwanafunzi ataapa na kuweka agano na Shetani mbele ya jopo la wachawi.

Baada ya hapo bila kuchelewa Shetani ataendelea na kusema kuwa hicho kiapo hakitoshi. Lakini mwanafunzi atakapouliza afanye kitu gani cha ziada, Shetani atahitaji kiapo kifuatacho kwa heshima yake na kwa heshima ya mashetani wote: Mwanafunzi ajikabidhi kwa Shetani kwa mwili na kwa roho yake yote daima dawamu, na afanye kila awezalo kuleta wanafunzi wengine wa kike na wa kiume katika ufalme wake. Kama hiyo haitoshi Shetani ataongeza kuwa lazima mwanafunzi atengeneze mafuta fulani kutokana na mifupa na viungo vya miili ya watoto, hasa watoto waliobatizwa, kwani kwa kufanya hivyo atamtimizia kila kitu atakachokitaka hapa duniani. Hiyo ni njia mojawapo ya kiapo.

Njia nyingine ya kiapo ni kwa wale ambao hawajiamini au wana hofu ya kuonana na Shetani uso kwa uso kilingeni, akiwa na mwili wa kimazingaombwe na sauti ya kutisha kwani Shetani hana mapafu wala hana ulimi. Badala ya kilingeni mwanafunzi hupelekwa kanisani na jopo la wachawi ambapo mbele ya jopo atalazimishwa kuikana imani yake, kumkana Yesu Kristo, kuukana ubatizo na kulikana kanisa zima kwa ujumla wake. Mwanafunzi baada ya hapo atalazimishwa kutoa heshima kuu kwa Mfalme Mdogo, kwani hivyo ndivyo wanavyomwita Shetani ili kumwondolea mwanafunzi hofu, kisha atalazimishwa kunywa supu ya mtoto mchanga waliyemuua akazikwa kisha wakamfukua na kupika viungo vya mwili wake; na dakika hiyo mwanafunzi atapata maarifa, maarifa ya kichawi, kama walimu wake na watarudi nyumbani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwa na mafanikio ya Shetani hayo si mafanikio ya kweli. Ukiwa na mafanikio ya Mungu hayo ndiyo mafanikio ya kweli. Mafanikio ya kweli hayatokani na NINI unacho. Mafanikio ya kweli yanatokana na NANI unaye. Yesu Kristo alikuwa maskini, hakuwa na kitu; lakini alikuwa tajiri, alikuwa na Mungu ndani ya moyo wake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kulinda heshima ya mfalme wao Yesu Kristo, kama Biblia na historia vinavyosema. Kwa nini watu (wengine) wa kizazi hiki wanasema hakuna Mungu na kwa sababu hiyo hawamwamini Yesu? Je, uko tayari kufa kwa ajili ya mtu aliyekufa kwa ajili yako? Kwa ajili ya mtu ambaye mitume walikuwa tayari kufa kwa ajili yake? Je, wewe una akili zaidi kuliko mitume? Yesu aliamua kufa ili wewe uishi, lakini bado unakuwa mbishi. Badilika.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama damu haina maana kwa nini Mungu anaipenda? Kama damu haina maana kwa nini Shetani anaipenda? Mungu ni roho, Shetani ni roho, lakini damu ni kitu kinachoonekana kwa macho. Kwa nini damu ni kitu cha muhimu kiasi hicho kwa Mungu na kwa Shetani pia? Damu ni pato la ziada la ufunuo wa kiroho. Yaani, damu ni sehemu ya ulimwengu wa roho. Mungu ndiye aliyetengeneza damu kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe, hata Shetani hajui kwa asilimia mia umuhimu wa damu katika ulimwengu unaoonekana na katika ulimwengu usioonekana. Damu ina uwezo wa kuzuia mapepo kutoka kuzimu yasiharibu mipango ya maisha ya watu na ina uwezo wa kuondoa dhambi. Kafara ya damu inapotolewa inaimarisha uhusiano kati ya mtu na ulimwengu wa roho. Roho unayoitolea kafara inasikiliza shida zako papo hapo na kila unachoomba aghlabu kinatekelezwa. Ukitoa kafara kwa ajili ya Shetani, Shetani atasikiliza shida zako. Ukitoa kafara kwa ajili ya Mungu, Mungu atasikiliza shida zako. Tatizo kubwa la mwanadamu ni dhambi! Jibu la tatizo hilo ni damu ya Yesu Kristo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa ‘Big Bang’, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi.

Wanaendelea kusema kuwa baada ya ‘Big Bang’ kutakuwepo na ‘Big Crunch’, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena.

Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa ‘Big Bang’ ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya ‘Big Crunch’, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia.

Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu – badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri – sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea.

Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa ‘dark matter’, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo ‘multiverse’ au ‘meta-universe’.

Kuna kitu kinaitwa ‘Higgs boson’ – chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (‘mass’) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa ‘Big Bang’ miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa ‘epoch’ – ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa ‘Big Bang’, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni.

Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya ‘dark matter’, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha ‘Standard Model’ litapatikana.

Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana ‘Higgs boson’ mwaka 1993 iliitwa ‘The God Particle’. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata.

Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo.

Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng’ombe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng’ombe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua.

Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho.

Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu.

Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia.

Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea.

Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea.

Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha ‘Joshua’s Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry’ kilichochapishwa mwaka 1890.

Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia – bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui.

Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hata hivyo, Shetani anaweza kutudanganya kupitia tamaduni zetu tulizozaliwa nazo. Utamaduni, dunia tunapoishi, ndiyo chanzo cha udanganyifu huu. Yesu Kristo alikufa msalabani ili tupate uhuru kutoka kwa Shetani. Chukua hatua sasa kwa sababu Shetani anaweza kukuteka, na kukufanya mtumwa tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Utajiri wa mbinguni ni wa milele na mungu wake ni Yehova. Utajiri wa duniani ni wa muda na mungu wake ni Mammon. Mammon, ambaye hata Yesu alimtaja katika Injili ya Mathayo 6 na katika Injili ya Luka 16, ni mungu wa uchoyo na utajiri wa dunia hii. Mammon kazi yake ni kufanya watu waliokufa kifedha na walio hai kifedha kuwa maskini wa milele ahera. Yesu Kristo alikuwa maskini, ili tuwe matajiri kupitia umaskini wake, lakini kwa sababu alikuwa na imani ya Mungu katika moyo wake alikuwa tajiri. Hivyo unaweza kuwa na utajiri wa mbinguni hapa duniani, ukiikaribisha amani ya Mungu katika moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu anaishi ndani ya damu, maisha ya Mungu yalikuwa yanaishi ndani ya mwili wa Yesu Kristo, anaishi ndani ya miili yetu. Unapokula damu, unapokunywa damu, unakula, unakunywa sehemu ya Mungu aliyekuumba.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mimi ni mwana wa Mungu. Sisi sote ni watoto wa Mungu. Lengo la kuzaliwa kwangu ni kufanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu na malaika kumtumikia Bwana, na kueneza injili ya Yesu Kristo duniani kote, kupitia vitabu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna aina tatu za upendo hapa ulimwenguni. Kuna upendo wa ‘agape’, upendo kati ya Mungu na binadamu na kati ya binadamu na binadamu mwenzake lakini hao binadamu shuruti wawe marafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Aidha kuna upendo wa ‘phileo’, upendo kati ya mtu na mtu au kati ya mtu na kitu au kati ya mtu na jambo; na kuna upendo wa ‘philadelphia’, upendo wa wanachama wa mashirika ya siri ambapo mtu humpenda mwenzake kama ndugu yake wakati si ndugu yake. Heri upendo wa ‘agape’ kuliko upendo ajmaina.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wengi tu vipofu wa kiroho! Ili tupone lazima tumtii na kumwamini Yesu Kristo, kama Yesu alivyomponya yule kipofu wa Siloamu kwa sababu alimtii na kumwamini, hata kama hatuwezi kuuona uso wake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sasa litambua hili: ushindi ni lazima kwa sababu Daudi wetu Yesu Kristo ameshamshinda Goliati wao Shetani. Amemshinda ili aishi ndani yetu na anaishi ndani yetu. Lakini hatutaweza kumshinda Shetani na malaika wake mpaka tutambue kuwa wapo na tuamini kuwa Mungu atawashinda kama tutampa nafasi ya kufanya hivyo kwa kuwa watiifu kwake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuona mambo ya rohoni lazima uwe na darubini ya imani. Darubini hiyo ni Yesu Kristo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu Kristo alilipa gharama ya maisha yake kutununua kutoka kwa Shetani. Alijitolea maisha yake ili wengine waweze kuishi. Upendwe vipi?”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna kocha wa maisha kama Yesu Kristo. Swali ni je, unakochika?”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mpinga Kristo atakapoona imeshindikana kuwanyamazisha, Eliya na Enock, huku akitamba kwamba yeye ndiye Yesu Kristo ambaye kila mtu ndiye aliyekuwa akimsubiri arudi kwa mara ya pili; na kwamba yeye anatoka katika ukoo wa mfalme Daudi, ili watu waamini kama kweli yeye ndiye Yesu Kristo, ataamuru Eliya na Enock wauwawe hadharani kama wahubiri wengine.

Eliya na Enock watakapouwawa, Mungu atawafufua na watarudi mbinguni wakiwa wameonja mauti kama binadamu mwingine yeyote yule. Hapo mlango wa rehema utakuwa umefungwa. Muda wowote kuanzia hapo Yesu atarudi, kwa mara ya pili, na kwa ajili ya ufufuo wa kwanza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika Biblia kuna tabiri 333 kuhusu maisha ya Yesu Kristo, na kuhusu kurudi kwake kwa mara ya pili. Kati ya hizo, 332 zilitimia! Bado mmoja tu: Kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili.

Unadhani huo wa kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili hautatimia? Muda umefika. Jitathmini katika maisha yako na uchague lililo jema.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu Kristo hakufa siku ya Ijumaa jioni na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi. Alikufa siku ya Jumatano jioni na kukufuka siku ya Jumamosi jioni. Wakati kifo kinamkumba, hakuwa na umri wa miaka 33, alikuwa na umri wa miaka 31. Kama Yesu Kristo alikufa siku ya Ijumaa jioni, na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi, hatuna Mwokozi!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu si wa kudhihakiwa (Wagalatia 6:7)! Katika maneno kadhaa ya Biblia, anasema bila masihara kabisa kwamba yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 34:14; Kumbukumbu la Torati 6:4-15) – Yeye si wa kuabudiwa kama mungu mwingine yeyote yule (Kumbukumbu la Torati 12:3-4, 30-31). Alipowaagiza watu wake wateule Israeli kwa njia ya ibada yake, aliwaonya wasiongeze juu ya kile alichokuwa amewapa wala wasipunguze chochote (Kumbukumbu la Torati 4:2; 12:32; angalia pia Ufunuo 22:18-19).

Kwa mfano, angalia hasira yake kuu wakati wana wa Israeli walipojaribu kumwabudu kupitia Ndama wa Dhahabu (Kutoka 32:1-9). Walitangaza kuwa ilikuwa sikukuu ya Bwana (mstali wa 5), lakini Mungu hakulithamini hilo! Alikuwa na hasira kali juu ya ibada ya sanamu za watu, kiasi kwamba alifikiria kuangamiza taifa zima na kuanza upya na familia ya Musa.

Mungu huyohuyo – Yahweh, Bwana wa Agano la Kale – akawa Yesu Kristo! Je, Mwokozi wetu atakubali kuabudiwa kwa namna yoyote ambayo misingi yake imejikita kwenye uongo? Hapana! Na hili kwa vyovyote vile limezingatia mila na desturi zisizo za kibiblia (labda tunaweza kusema za “kipagani”) ambazo zimechukua nafasi ya maadhimisho ya kafara na ushindi wa kishindo wa Yesu Kristo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Manabii wa uongo, na wafuasi wao, hawautaki ukweli. Kazi yao ni kutulazimisha tumwabudu Mpinga Kristo, badala ya Yesu Kristo, bila sisi wenyewe kujua. Wana mamlaka yote ya Mpinga Kristo kwa sababu, kama Mpinga Kristo, wanaongozwa na Shetani. Walimu hawa wa uongo wanaopenda kuvalia misurupwenye ya kisawasawa, na wanaoongea utafikiri wamemeza Biblia na kuitapika kwenye mikrofoni, lengo lao ni kutupeleka kwenye ufalme wa Shetani. Hatuna budi kuitangaza injili ya kweli ya Yesu Kristo, kwa imani ya kweli, kupata urithi usiohongeka wa ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote mbele ya Yesu Kristo.”
Enock Maregesi

« previous 1
All Quotes | My Quotes | Add A Quote