Tabia Quotes

Quotes tagged as "tabia" Showing 1-10 of 10
Enock Maregesi
“Nukuu ya mwandishi wa vitabu wa Brazili, Paulo Coelho, "Tunapopenda tunajitahidi siku zote kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo. Tunapojitahidi kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo, kila kitu katika maisha yetu kinakuwa kizuri hali kadhalika.", inadhihirisha kikamilifu tabia ambayo bibi yangu (Martha Maregesi) alijitahidi kuwa nayo katika kipindi cha maisha yake yote. Alikuwa mtu mwenye furaha sana. Alikuwa na tabasamu lenye kuambukiza ambalo marafiki na familia yake hawakuweza kujizuia kutabasamu pia alipofurahi nao. Pamoja na kwamba alikumbana na matatizo mengi na bahati mbaya nyingi katika maisha yake, alijulikana kama mtu mwenye upendo na uvumilivu mkubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Familia yako haikusaidii chochote katika mipango ya takdiri yako. Hii inasikitisha sana. Unajitahidi kila siku kuwafurahisha watu unaowapenda na watu wako wa karibu. Kila ukijitahidi kupata kibali cha watu unaishia kudharaulika na kuonekana mjinga asiyekuwa na maana. Sikiliza mazungumzo ya ndani ya moyo wako. Wapendwa wako watakukubali kama mtu hodari asiyekata tamaa, na tena watakuheshimu kutokana na tabia zako hizo. Mabadiliko haya ya kifikra hayatatokea haraka kama unavyofikiria. Yatachukua muda. Hivyo, kuwa mvumilivu. Wakati huohuo, endelea kucheza ngoma uliyoianzisha mwenyewe, endelea na mipango yako kama akili yako inavyokutuma.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Badilisha tabia. Badilisha mazingira ya maisha yako. Haijalishi una umri kiasi gani au wewe ni mwanamke au mwanamume, bado hujachelewa kubadili maisha yako kutoka duni kuwa bora – kuwa na amani, furaha na kuridhika. Kama desturi yako ni kuamka saa 12:00 asubuhi kila siku ili ufike kazini saa 2:00 asubuhi ambao ni muda wa serikali wa kuanza kazi, amka saa 11:30 asubuhi ili ufike kazini saa 1:30 asubuhi – nusu saa kabla ya kuanza kazi. Kama unafanya kazi ya taaluma uliyosomea lakini maisha hayaendi, fikiria kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma kufikia malengo uliyojiwekea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema – sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sina nyemi na mwanamke mwenye sura nzuri na tabia mbaya. Nina nyemi na mwanamke mwenye sura mbaya na tabia nzuri, au mwanamke mwenye sura nzuri na tabia nzuri. Mwanamke wa kuoa sitampenda nitampendelea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kila mtu ana tabia, matendo, mawazo na akili yake tofauti na mtu mwingine hapa duniani. Usimdharau mtu ukidhani ana akili kama za kwako au anafikiri kama unavyofikiri wewe kwani kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Unaweza kudhani unamjua mtu kumbe humjui. Heshimu kila mtu kama unavyojiheshimu kwa sababu, kila mtu ni wa pekee. Kama tunavyotofautiana katika vidole na macho ndivyo tunavyotofautiana katika tabia, matendo, mawazo, imani, maadili na akili. Usimdharau mtu usiyemjua au unayedhani unamjua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Marafiki wanaweza kukupotosha bila wao wenyewe kujua na bila kuwa na nia mbaya ya aina yoyote ile; na wanaweza kuwa washauri wazuri kwa sababu wanakujua vizuri unapokuwa na huzuni, na wanakujua vizuri unapokuwa na furaha pia. Kwa mfano; rafiki yako anaweza kukushauri kusomea uhasibu wakati Mungu amekupangia utawala, au anaweza kujua aongee na wewe wakati gani kulingana na tabia yako ya kubadilikabadilika. Maadui wanasaidia kujua kipaji ulichopewa na Mungu – ukifanya kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yako halafu ukawa na maadui ujue hicho ndicho Mungu alichokupangia kufanya, hivyo usikate tamaa – na mashabiki wanasaidia kufanya kipaji chako kiwe na uhai.”
Enock Maregesi

“Tabia ya mwanamke mwema inapaswa kufichwa ndani ya Kristo ili mwanamume anayemtaka huyo mwanamke amtafute ndani Kristo kwanza, ili kukutana naye.”
Wilson M. Mukama

Enock Maregesi
“Tabia yako ya siri mwanao atakuwa nayo! Kama Nelson Mandela alikuwa alama ya msamaha, msamaha ni tabia yetu. Kama Kwame Nkrumah alikuwa alama ya umoja, umoja ni tabia yetu. Kama Patrice Lumumba alikuwa alama ya uzalendo, uzalendo ni tabia yetu. Kama Robert Mugabe ni alama ya udikteta, udikteta ni tabia yetu. Kama Haile Selassie alikuwa alama ya ushujaa, ushujaa ni tabia yetu. Kama Samora Machel alikuwa alama ya ujamaa, ujamaa ni tabia yetu. Kama Julius Kambarage Nyerere alikuwa alama ya haki, haki ni tabia yetu. Sisi ni watoto wa wazalendo wa Afrika! Wao ni baba wa mataifa ya Afrika! Tumerithi tabia zao za siri.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tabia yako inayofanya mtu akuchukie ichukie.”
Enock Maregesi