Kujitolea Quotes

Quotes tagged as "kujitolea" Showing 1-7 of 7
Enock Maregesi
“Jina langu ni Enock Maregesi na ningependa kukwambia kisa kidogo kuhusiana na bibi yangu, Martha Maregesi. Mwanamke huyu alikuwa mke mwenye upendo usiokuwa na masharti yoyote. Alikuwa mama na bibi aliyefundisha familia yake umuhimu wa kujitolea na umuhimu wa uvumilivu. Ijapokuwa hakupendelea sana kujizungumzia mwenyewe, ningependa kukusimulia kisa kidogo kuhusiana na hadithi ya maisha ya mwanamke huyu wa ajabu katika maisha yangu.

Bibi yangu alizaliwa katika Kitongoji cha Butimba, Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi, Tarafa ya Nyanja (Majita), Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, katika familia ya watoto kumi, mwaka 1930. Alisoma katika Shule ya Msingi ya Kome ambako alipata elimu ya awali na msingi na pia elimu ya kiroho kwani shule yao ilikuwa ya madhehebu ya Kisabato. Aliolewa na Bwana Maregesi Musyangi Sabi mwaka 1946, na kufanikiwa kupata watoto watatu; wa kiume wakiwa wawili na wa kike mmoja. Matatizo hasa ya bibi yalianza mwaka 2005, alipougua kiharusi akiwa nyumbani kwake huko Musoma. Hata hivyo alitibiwa hapo Musoma na Dar es Salaam akapona na kuwa mwenye afya ya kawaida. Lakini tarehe 19/10/2014 alipatwa tena na kiharusi na kulazwa tena katika Hospitali ya Mkoa ya Musoma, ila akajisikia nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani – lakini kwa maagizo ya daktari ya kuendelea na dawa akiwa nje ya hospitali. Tarehe 29/10/2014 alirudi tena Hospitali ya Mkoa ya Musoma kwa tiba zaidi, lakini tarehe 4/11/2014 saa 7:55 usiku akafariki dunia; akiwa amezungukwa na familia yake.

Dunia ina watu wachache sana wenye matumaini na misimamo ya kutegemea mazuri, na wachache zaidi ambao wako tayari kugawa matumaini na misimamo hiyo kwa watu wengine. Nitajisikia furaha siku zote kwamba miongoni mwa watu hao wachache, hata bibi yangu alikuwemo. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake. Kwa kuwa bibi yangu ametanguliwa na msalaba, msalaba utamwongoza mahali pa kwenda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mama anaweza kufa ili mwanawe aishi, anaweza kufunga na kuomba ili mwanawe Mungu amsaidie ashinde mtihani wake, anaweza kulala njaa ili mwanawe ale, anaweza kujitolea vitu vingi au mambo mengi katika maisha yake ili mwanawe aishi vizuri, anaweza kuingia dhambini ili mwanawe asamehewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Silaha kuu ya uchoyo ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ni upendo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu alimpa kila mmoja wetu vipawa na vipaji vya pekee kwa ajili ya huduma yake. Kazi yake kwetu hapa duniani ni kutumia vipawa na vipaji vyetu kwa ajili ya huduma ya watu wengine. Kila mmoja wetu ana kitu fulani anachoweza kutoa kwa ajili ya mtu mwingine mwenye shida. Tunaweza kutoa pesa zetu na muda wetu kwa watu maskini. Tunaweza kuwa marafiki kwa watu wapweke au watu wasiojiweza kiafya. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea kwa ajili ya mabadiliko ya watu wengine. Tunaweza kuwa wasuluhishi wa migogoro ya amani. Tunaweza kuwa na upendo usiokuwa na masharti yoyote kwa familia zetu. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea au kazi za kuajiriwa kwa uadilifu, uaminifu, heshima, na upendo kwa wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kujitolea kwa moyo mmoja kwa muda mrefu huleta furaha na afya njema kwa mtoaji na kwa mpokeaji pia.”
Enock Maregesi